PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha  ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoani Dodoma akiambatana na Viongozi wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wengine  katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiangalia Mchanga aina ya Phosphete unaotumika kutoa sumu kwenye udongo kabla ya kupanda mazao. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha Itracom Fertilizer Limited wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiangalia mbolea ambayo imefungashwa alipotembelea kiwanda  cha mbolea cha  ITRACOM Fertilizer Limited kilichopo Dodoma.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited, Kimaramuziro Nkurikiye akitoa taarifa kuhusu kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) katika kiwanda hicho Mkoani Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha  ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea  kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM.

Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya  wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea  umezalisha  ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za  kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati  na kuwa na  tija kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.

Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri pamoja na viongozi na watendaji yake na Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *