NDEJEMBI ASISITIZA UWAJIBIKAJI KWA WATAALAM WA ELIMU

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deogratius John Ndejembi amewahimiza Wataalamu wa Idara ya Elimu kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo leo wakati wa kikao kazi wa Wataalamu wa idara Elimu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

“Hatutamuelewa mtumishi yeyote ambaye hatosimamia fedha za miradi vizuri kwa maana hakuna (investment)kubwa iliyowahi kufanyika kama kipindi hiki cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi ndio tupo kukamilisha historia hiyo ya hiyo na fedha nyingi bado inaendelea kuletwa tunategemea kupokea zingine muda si mrefu kama hatusimamii vizuri huko chini hakuna kitu kitakachoonekana amesema Mhe. Ndejembi

Aidha, Mhe. Ndejembi amewahimiza watumishi hao kuwasimamia vizuri walimu kwa kujenga mahusiano mazuri ikiwemo kutoa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri na kusisitisa kuhusu kuwathamini walimu ili kuwapa hamasa ya kufanyakazi kwa bidii.

“Tuhakikishe tunatoa huduma kwa haraka kwa watumishi wetu hasa walimu ambao ndio jeshi kubwa tunalitegemea ni lazima tumjali tunaona Mhe. Rais kwakujali yeye alifanya makubwa kwa kutoa (Promotion) walimu wengi walikuwa wanalia (Promotion) hicho kilio amekiondoa hakipo tena sasa kwenye hivi vidogo vidogo tumsaidie Mhe. Rais” Mhe. Deo Ndejembi amesisitiza hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *