
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Alhaj Jabir Shekimweri na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde wamekutana kwa pamoja na wananchi wa Mtaa wa Mahomanyika kata ya Nzuguni kwa ajili ya kusikiliza na kutoa uamuzi wa mgogoro wa ardhi wa eneo la ukanda wa kijani uliodumu kwa miaka mingi baina ya wananchi na Jiji la Dodoma.
Maamuzi hayo yamefanywa kufuatia kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Mbunge Mavunde na Diwani wa kata ya Nzuguni Mh. Alloyce Luhega

Akitoa maelezo ya awali Diwani wa kata ya Nzuguni Mh. Alloyce Luhega amesema kwamba mgogoro wa ardhi wa ukanda wa kijani umekuwa ni changamoto kubwa ka maendeleo ya mtaa huo na kwamba wananchi wanasubiri maamuzi ya serikali ili waweze kujipanga kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde alisema kwamba wananchi wa Mahomanyika wana matatizo makubwa matatu kwa sasa;
1.Ukarabati wa miundombinu ya mtandao wa maji kuwafikia wananchi wote.
Hapa zinahitajika 101m na mimi nitashirikiana na Wizara ya Maji kuhakikisha mtandao huu unakamilika,lakini pia mwezi wa Oktob DUWASA watachimba visima viwili vya maji.
2.Mgogoro wa Ardhi Ukanda wa Kijani.
Mgogoro huu umedumu kwa muda mrefu naiomba serikali ya Wilaya leo ifanye maamuzi ili wananchi wangu waishi kwa amani na furaha katika ardhi hii waliyijaaliwa na Mwenye Mungu.
- Eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha CSR ya Mradi wa Outer Ring Road
Kumekuwa na mvutano juu ya wapi pajengwe kituo cha Afya,Mh DC naomba kama ambavyo imetamkwa na wahusika wa mradi kituo hichi kijengwe Mahomanyika na si eneo lingine.
Akijibu hoja hizo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma *Mh. Alhaj Jabir Shekimweri * amesema ni maelekezo ya *Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan * kwamba viongozi watatue kero za msingi za wananchi na hivyo ametumia fursa hiyo kuliagiza Jiji la Dodoma kuharakisha upangaji na umilikishwaji wa wananchi katika eneo hilo na kulipanga kisasa iki liendane na sifa ya Makao Makuu.
Na pia ameelekeza kituo cha Afya kijengwe Mahomanyika na si Nzuguni kama ilivyokuwa awali,kwak kuwa kuna mradi mwingine mkubwa wa zaidi Tsh 2bn wa ujenzi wa kituo cha Afya karibu na eneo la Nzuguni C ambapo wananchi hao watapata huduma