SERIKALI KUTAMBUA NA KUENDELEZA BUNIFU ZA WATANZANIA NA WANAFUNZI VYUONI

Na Deborah Munisi – Dodoma

Serikali inatambua bunifu za wanafunzi na watu mbalimbali zinazofanywa kwa kuzitambua, kufanya majaribio na hatimaye kuanza kutumika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda Wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saasisha Mafuwe alilotaka kujua mikakati na mpango wa serikali katika kutambua na kuendeleza bunifu za wanafunzi vyuoni alilouliza kuwa,


“Serikali inampango gani wa kutambua na kuendeleza bunifu zinazofanyanywa na wanafunzi vyuoni hapa nchini ili waendelezwe na Serikali ikiwemo chuo cha DIT Kuna mwanafunzi aliyetengeneza Mfumo wa kucontrol makosa ya barabarani” Mhe. Mafuwe

“Zipo bunifu ambazo zimeanza kutambulika zinafahamika na hatua zilizobaki ni kuhakikisha bunifu hizo zinaingia sokoni, kwa mfano bunifu ya kuweza kulipia bili ya maji kwa kutumia simu janja ambayo imegunduliwa na Mtanzania na kwasasa inafanyiwa majaribio kwaajili ya kununuliwa na Mamlaka ya Maji Tanzania na kutumika” Prof. Mkenda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *