WAWEKEZAJI WAKARIBISHWA KUWEKEZA KILIMO CHA VANILA ARUSHA

WAWEKEZAJI Jijini Arusha, wamehimizwa kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla ili waweze kujikwamua kwa kupata kipato kitakachoweza kuwainua na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Vanilla Village Arusha, Joyce Adam chini ya Kampuni ya Vanilla Internation wakati wa kutembelea shamba la Vanilla lililopo eneo la Ndunduma Songambele, Arusha.

Ambapo amesema:
“Wawekezaji wa zao la Vanilla wameweza kujionea uwekezaji wa zao la Vanilla

Zao hili halina gharama kubwa hivyo ni fursa za kiuchumi na pia ni kilimo chenye uhakika, wale wawekezaji wadogo wadogo, wa kati na wakubwa tunawakaribisha Vanilla Arusha. ” Amesema Joyce Adam.

Aidha, amesema zao hilo kuwa na bei kubwa kutokana na matumizi yake ikiwemo dawa za magonjwa kama Kisukari, magonjwa ya moyo, Kansa na mengine.

“Vanilla ni zao lenye kumpa mkulima faida kubwa. Inatumika katika viungo, pia ladha mbalimbali kama chocolate, ice cream
Lakini pia inasaidia kukuza kumbukumbu, na masuala mengine kwa mwili wa binadamu ” amesema.

Na kuongeza kuwa, bei ya kilo moja ya Vanilla ni milioni moja, hivyo mkulima kunufaika kwa matumizi na kiuchumi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliotembelea kwa namna ya kujifunza na kuwekeza kwenye zao hilo, wameshuhudia hatua za ukuaji wa zao na namna inavyokuwa shambani

Joshua Michael ni mmoja wa vijana ambaye amevutika katika kuwekeza kwenye zao hilo Jijini Arusha Ambapo ameelezea Kufurahia zao hilo kwani anaamini litaenda kukua ukuaji wa uchumi kwa vijana.

Nae Dikson Sawe, amesema amekuwa na shauku ya kubwa katika kuwekeza kwenye Kilimo, hivyo kupata kwake kwa elimu ya uwekezaji na kushuhudia shamba hilo la vanilla imempa nguvu ya kuweza kuendelea kuingia kuwekeza .

Nae Sophia Sebastian mkazi wa Arusha, ametoa wito kwa Wanawake kujitokeza kuwekeza kwenye zao hilo.

Sophia ametoa wito kwa wanawake wenzake kuingia kwenye Kilimo hicho kwani ni kilimo chenye manufaa makubwa kiuchumi.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla Internation, Simon Mnkondya amesema Kilimo cha zao la Vanilla ni miongoni wa fursa ambayo ni adhimu na inayohitajika duniani hivyo jamii ikijikita katika kilimo hicho inaweza kujikwamua kiuchumi.

“Asilimia 60 ya wafanyakazi katika kampuni yetu ni wasichana ambao wametelekezwa na wanaume zao ambapo kwa mujibu wa utafiti tulioufanya tumebaini wanasichana hawa ni wavumilivu Sana. “Amesema Mnkondya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *