NDEGE MPYA YA MIZIGO TANZANIA KUNUFAISHA WAFANYABIASHARA NCHINI

Na Deborah Munisi – Dar Es Salaam

Ndege Mpya ya mizigo ya Air Tanzania Boeing B767-300F imewasili katika uwanja wa Ndege cha Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo Juni 3, 2023 na kupokelewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan


Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 54 za mzigo ikiwa ni sawa na malori matano na nusu ya tani kumikumi ambayo pia ina uwezo wa kusafiri kilometa 11,070 angani bila kutua kuongeza mafuta hii ikiwa na maana kuwa ni sawa na kusafiri muda wa saa 10 bila kutua.

Ikumbukwe kuwa hii ndiyo ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767 -300F June 03,2023 yenye uwezo mkubwa huku matarajio ya Serikali ni kutatua changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa Wafanyabiashara nchini kwa kusafirisha kwa gharama nafuu na kwa urahisi.


Miongoni mwa sifa za ndege hii ni kwamba Matanki yake ya mafuta yana uwezo kubeba lita 90,770, mabawa yake yakiwa na urefu wa meta 47.6, pia inaweza kwenda mwendokasi wa kilometa 850 kwa saa na ina urefu wa meta 54.9.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *