Na Deborah Munisi, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametoa Maagizo Kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Wote nchini kwenye Halmashauri zao Kusimamia Kutokuwepo kwa Michango Holela inayo kera Wananchi na kushindwa kufanya Shughuli nyingine hali inayopelekea Wanafunzi kuondolewa mashuleni.
Mhe. Majaliwa Ameyasema hayo Leo Jun 1,2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Ally Kasinge alilotaka kujua “Je Serikali haioni Umuhimu wa kupitia sera ya Elimu bila malipo ili michango ya Ulinzi, Shajala pamoja na michango ya Chakula iwe ni jukumu la serikali kwa dhana ile ile ya kuwapunguzia gharama wazazi au walezi” Mhe. Kasinge

Majaliwa amesema serikali inaendelea kutekeleza Sera ya Elimu bila Malipo (bila Ada) kwa lengo la kuwapunguzia wazazi michango mingi ambayo ni holela na kuleta usumbufu ambapo amesema serikali hupeleka fedha kwenye Kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule.
“Serikali inapeleka fedha kila Mwenzi kwenye kila Halmashauri kwaajili ya kuwezesha shule zetu za sekondari, Wakuu wa shule na uongozi wa shule kuweza kutumia kwenye maeneo ambayo walitarajia sana kupata michango kutoka kwa Wazazi” Mhe. Majaliwa
