TANZANIA NA JAPAN KUSHIRIKIANA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

Na Eleuteri Mangi

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi zaidi hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Bw. Yakubu amesema katika kikao chake na Mtaalamu wa michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) Dkt. Shiraishi Tomoya Juni 01, 2023 jijini Dodoma.

“Uwepo wako hapa nchini utasaidia wananchi kuwaokoa na watu wengi na magonjwa yasiyoambukiza, Rais yupo mstari wa mbele katika michezo, naamini uwepo wako hapa nchini butasaidia kukuza michezo na kuifanya kuwa maarufu na watu wengi kushiriki” amesema Bw. Yakubu.

Kwa upande wake Dkt. Shiraishi Tomoya amesema anauzoefu wan chi za Afrika Mashariki na anaiona michezo katika miaka 10 ijayo michezo inakuwa sehemu ya jamii ambapo watu wote watashiriki na kuimarisha afya zao.

Dkt. Shiraishi Tomoya ni mtaalamu na mshauri wa michezo na maendeleo atakuwepo nchini na kufanya kazi katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atakuwa nchini kwa muda wa miaka mitatu kutoka 2023 hadi 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *