TAMISEMI NA WIZARA YA UJENZI KUFANYA TATHIMINI YA KUPANDISHA HADHI BARABARA ZA MKOA WA KILIMANJARO

Kama lilivyotakwa la kisheria vikao vyote vinavyokaa katika ngazi ya Wilaya na Mkoa zinafikishwa kwa Waziri Mwenye dhamana TAMISEMI na Wizara ya ujenzi zitakaa kuona ni hatua zipi ambazo zimefikiwa za kupandisha hadhi barabara za Mkoa wa Kilimanjaro.

Ni kufuatia swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saasisha Mafuwe akitaka majibu ya serikali ikiwa ni kufuatia kikao cha barabara cha Mkoa wa Kilimanjaro na kikao cha RCC Mkoa na tayari alishawasilisha Wizarani kilichokaa na kupitisha barabara kadhaa tangu mwaka juzi ili kupandishwa hadhi kutoka TARURA kwenda TANROAD.

” Je? ni lini barabara hizo zitapandishwa hadhi kutoka TARURA kwenda TANROAD? Mhe. Mafuwe

Akitoa majibu ya swali Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi ameonyesha kuwa na utayari wa kukaa na Wizara ya ujenzi ili kuona hatua zilizofikiwa na hatimaye kuzipandisha hadhi.

“Kama lilivyotakwa la kisheria vikao vyote vinavyokaa katika ngazi ya Wilaya na Mkoa zinafikishwa kwa Waziri Mwenye dhamana ambaye ni Waziri wa ujenzi hivyo TAMISEMI na Wizara ya ujenzi zitakaa kuona ni hatua zipi ambazo zimefikiwa za kupandisha hadhi barabara za Mkoa wa Kilimanjaro” Mhe. Ndejembi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *