CHUO CHA TAALUMA POLISI DSM CHATOA MAFUNZO KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kimeendelea kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

Akitoa taarifa hiyo leo Mei 30,20223 Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema kuwa chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali wawapo chuoni hapo.

Ameendelea kueleza kuwa lengo la kutoa elimu hiyo ni kujenga uwezo kwa maofisa,wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi hilo na makundi mengine ya wahitaji ambapo amebainisha kuwa ni vyema kila askari kuwa na vifaa wezeshi ili kukabiliana na majanga hayo pindi yanapotokea.

Mbali na hilo Mkuu wa chuo hicho ametumia fursa hiyo kumpa pole mkufunzi wa chuoni hapo aliyepata majanga ya kuunguliwa moto nyumba yake, ambapo amebainisha kuwa kutokana na changamoto hiyo aliyoipata waliona vyema kuungana kama Jumuiya ya Chuo cha Taaluma ya Polisi kumpa Mkono wa Pole kwa kadhia aliyoipata.

Kwa upande wake Sajenti Saidi Hamad aliyepata janga hilo la kuunguliwa moto nyumba yake ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kwa namna walivyoguswa na tukio hilo, ameongeza kuwa nyumba yake iliyopo Zanzibar iliteketea yote kwa moto ambapo anamshukuru Mungu familia imebaki salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *