SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA KATA YA KIA, MUUNGANO, MNADANI, UROKI NA WERUWERU KATIKA HALMASHAURI YA HAI

Serikali kupitia ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa imedhamiria kujenga vituo vya Afya Kata ya KIA, Muungano, Mnadani, uroki na Weruweru katika Halmashauri ya Hai na kutoa maagizo kwa mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kufanya tathimini za kina ili kukithi vigezo vya kupandishwa hadhi na kuwa vituo vya afya.

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saasisha Mafuwe alilouliza Leo Mei 29, 2023 bungeni jijini dodoma ikiwa ni kufuatia kitendo cha wananchi kutembea umbali mrefu kutoka katika kata zao kufata huduma Bomang’ombe.

“Kata ya KIA,Muungano,Mnadani, uroki na Weruweru hazina vituo vya afya na wananchi wanatembea umbali mrefu sana kufata huduma Bomang’ombe Je? ni lini Serikali itajenga vituo vya afya kwenye kata hizi muhimu?” Mhe. Mafuwe

Aidha Naibu waziri Ndejembi amesema serikali itatekeleza ukamilishaji wa ujenzi huo kadri ya upatikanaji wa fedha ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa Jimbo hilo badala ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *