
“Tuondoe migogoro kwenye maeneo yetu, tumeona na tunajua faida ya upangaji bora matumizi ya ardhi, watu wanauwana sababu ya migogoro ya Ardhi na nafikiri hii migogoro huenda inanufaisha Wizara” Mhe. Mwaifunga
Ni Mbunge wa viti maalumu Mhe. Hawa Mwaifunga wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi na Maliasili Leo Mei 26, 2023 bungeni jijini Dodoma ambapo amesema ipo haja ya kubeba mkopo wenye manufaa kwa Watanzania.
“Kama hakuna manufaa lazima wafike mahali wajue migogoro ya ardhi inatosha” Mhe. Mwaifunga

“Kama unapewa mkopo na unaona hayana manufaa kwa Watanzania unabeba wanini?, Kwanini mkopo huu usiwasaidie Watanzania huko walipo?, Kama Watanzania wanauwana kwenye migogoro ya Ardhi nani atakwenda kwenye hayo majengo mnayoyajenga?” Mhe. Mwaifunga
Ikumbukwe kuwa Mbunge Mwaifunga ni miongoni mwa wabunge wengi waliotoa michango yao ya kuitaka Wizara kutatua migogoro ya ardhi iliyopo na baada ya hoja hizo ukafika wakati wa Waziri wa wizara hiyo Mhe. Angeline Mabula kujibu hoja.

Waziri Mabula amesema kuwa usugu wa migogoro hiyo hutokana na viongozi kuanzia ngazi ya chini kutotatua migogoro kwa wakati na hatimaye kukomaa na kuwa sugu.
“Tukianza kutatua migogoro hii kuanzia ngazi za chini tutaepuka haya, wananchi waheshimu mipaka iliyowekwa kwani akivunja mipaka ataonekana mhalifu tu” Waziri Mabula