MGOGORO WA MTINGA- TANZANIA NA KENYA BADO NI KIZUNGUMKUTI

Serikali imetakiwa kufanya hima kutatua mgogoro uliopo baina ya mpaka wa Tanzania Wilaya ya Mtinga Mkoani Tanga na Kenya kwani umekuwa ni wa muda mrefu hali inayopelekea kuwepo kwa mwingiliano mbovu ambao unaathiri shughuli za kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mkinga Mhe. Dastan Kitandula wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi na Maliasili Leo Mei 26, 2023 bungeni jijini Dodoma.

“Changamoto ya mpaka wa Tanzania na Kenya, wenzetu wa vyombo vya ulinzi Kenya wanafika mpaka maeneo ya ndani ya Kijiji chetu wakiwa na silaha kama isingekuwa hekima za viongozi wetu tungeingia kwenye migogoro” Mhe. Kitandula

“Naiomba serikali yangu itusikie, walisaini document ya makubaliano lakini baada ya makubaliano hayo Bado kumekuwa na chokochoko za jeshi la ulinzi la Kenya kuingia kwenye maeneo yetu lakini wananchi wetu walipoingia walikamatwa baharini wakaenda kufunguliwa kesi na kutaifishwa Mali zao” Mhe. Kitandula

Sanjari na hayo amesema ni Vyema serikali kuvalia njuga usalama wa mpaka huo kabla ya kuleta madhara baadaye.

“Tusiache kuchukua hatua watu wetu badala ya kwenda kuhukumiwa Kenya ikafika mahali vyombo vyao vikazamishwa baharini tukapoteza maisha ya watu” Mhe. Kitandula

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *