
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe. Saputu Noa ameitaka serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maliasili kutoa baraza la Ardhi chini ya Wizara na kulipeleka chini ya mahakama kwa lengo la kumtimizia mwananchi wake haki kwa wakati.
Ameyasema hayo Leo Mei 26, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi na Maliasili iliyowasilishwa Bungeni hapo ambapo piah ameisisitiza Wizara kutoa tamko kwa makampuni yanayohusika kupimia Ardhi ili wananchi wanufaike na huduma hiyo.
“Kwanini tunaendelea kung’ang’ania mabaraza chini ya Wizara? Bora yawekwe chini ya majakama ili kutoa haki kwa Watanzania” Mhe. Noa

“Waziri toa tamko kwa makampuni ambayo yamepimia wananchi Ardhi, imepelekea wananchi kupata matatizo makampuni yamekimbia” Mhe. Noa
Aidha amesema ipo haja ya kuboreshwa kwa Sheria ya ardhi ili itoe haki kwa wakati kwa raza hayo yasiwakandamize wananchi ambapo amependekeza kuwa siyo sahihi wageni kimilikishwa Ardhi.

“Hii siyo sawa wageni kumiliki Ardhi, haki iliyochelewa ni sawa na haki iliyonyimwa” Mhe. Noa
“Wananchi wanakutegemea kutoa haki, Sheria ya Ardhi na mabaraza yaboreshwe kwani yanamkandamiza mwananchi ” Mhe. Noa