UJENZI WA BARABARA SITA KIWANGO CHA LA MIKUKAMILISHWA JIMBO LA HAI

Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe amefurahishwa na zoezi la wakandarasi kuwa site katika utekelezaji wa barabara Sita kwa kiwango cha lami na nyingine za kiwango cha changarawe zinazoendelea kukamilishwa katika Jimbo hilo kwani ni dhahiri shahiri serikali inatekeleza kwa vitendo zoezi hilo.

Ametumia nafasi hiyo Kumshukuru Mungu kwa hatua hiyo kubwa ya kimaendeleo na Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassani kwa utekelezaji huo.

“Mkisikia ninamshukuru Mungu na Mhe Rais wetu Jamani mnielewe yaani wakandarasi wapo site sasa hivi Barabara sita kwa kiwango cha Lami na nyingine kibao kiwango cha changarawe na bado Bajeti hii mzigo wa kutosha unakuja Sifa na utukufu kwa Mungu wetu barabara ya Makoa – Tacri – Mferejini 7km, Bomang’ombe-Rundugai-Kikavuchini 0.5Km, Nyerere road 0.79Km, Stand-Kingereka 0.2km na St. Dorcas-Relini 0.34km ujenzi unaendelea pia barabara ya Ttcl-Rc Church 0.475km” Mhe. Mafuwe

Katikarahisisha upatikanaji wa Maendeleo katika Jimbo hilo Ikumbukwe kuwa Mbunge huyo Mei 24, 2023 bungeni jijini Dodoma alisimama na kuomba wajengewe km7 barabara ya Mjengweni Sirinjoro itakayo rahisisha shughuli za usafirishaji na kiuchumi Mkoani humo.

Kufuatia ombi hilo serikali imeahidi kutekeleza hilo kadri ya upatikanaji wa fedha Ili wananchi wapate miundombinu bora.

Matukio katika Picha Kinachoendelea Jimbo la Hai wakati zoezi la ujenzi wa ukamilishwaji wa Barabara Sita zinazoendelea kujengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *