“TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI CHACHE DUNIANI ZENYE AMANI NA WANANCHI WAKE WANAISHI KWA RAHA” MHE. AHMED

“Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Afrika na duniani ambazo mpaka sasa hivi Ina amani na tunaishi kwa raha, iwe ni wafanyabiashara, wafanyakazi na Watanzania ambapo Moja ya sababu kubwa ni uwepo wa jeshi letu ambalo wanafanya kazi usiku na mchana” Mhe. Ahmed


Ni Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum wakati akichangia bajeti ya Wizara ya ulinzi na jeshia kujenga Taifa hotuba iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo Mhe Innocent Bashungwa Leo Mei 24, 2023 bungeni jijini Dodoma.

Ametoa pongezi kwa majeshi yote hapa nchini kwa kujitoa kwao muhanga na kutoa maisha yao kwaajili ya kulinda amani ya nchi huku akitoa ushauri kwa serikali kuweka mipango mikakati ya kuboresha majeshi kuwa ya kisasa zaidi.


“Miliwahi kusikia huko Kusini Kuna wakati ilitokea taharuki ya hapa na pale kazi kubwa ilifanywa na jeshi letu la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kuna vijana kule wamekaa kwenye mapori mazito ambao wako tayari kujitoa muhanga na kutoa maisha yao kwa ajili ya Muungano wa Tanzania” Mhe. Ahmed

“Upo umuhimu wa kuweka mpango wa kuboresha jeshi la Tanzania kutoka hapa tulipo na kuwa katika Moja ya jeshi Bora Afrika kwa kubadilisha mitambo, kuboresha mawasiliano na jeshi likawa la kisasa zaidi” Mhe. Ahmed


Hata hivyo amehitimisha kwa kuunga mkono kipengele cha kushirikisha sekta binafsi katika kuliendeleza jeshi.


“Tutaingia partner ship na sekta binafsi katika kuliendeleza jeshi, wapo wenye uwezo mkubwa sana, mainjinia wazuri hivyo ni swala la kukaa na kuwa na mipango Ili kama zimekuja sekta binafsi waziri leta tuzupitishe hapa bungeni”. Mhe. Ahmed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *