SERIKALI YATAKIWA KUTILIA MKAZO KWA VIJANA MAFUNZO YA JKT NA JKU

Serikali yahimizwa kutilia mkazo swala la vijana kwenda kwenda kwenye mafunzo ya JKT na JKU ili kuwajengea ukakamavu, maadili na uzalendo kwa taifa na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.
Hayo yamesemwa ya Mbunge wa Jesca Msambatavangu Mei 24, 2023 bungeni jijini dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa iliyowasilishwa na baadaye kupitishwa bungeni hapo.


“Yapo mambo mengi yanatuchanganya akili na hatujui tunafanya nini kumbe vipo vyombo ambavyo hatujavitumia sawa sawa na kama tungevitumia matatizo yanayotukosesha usingizi mambo kama ajira kwa vijana, maadili kwenye Taifa letu uzalendo na ukakamavu” Mhe. Msambatavangu


“Serikali inatakiwa kuongeza idadi ya kambi za JKT na JKU ili kuwezesha vijana wengi wakiwemo wahitimu wote wa kidato cha sita, tunataka hilo ongezeko kubwa la vijana wa mtaani waende JKT”Mhe. Msambatavangu

Aidha ametumia nafasi kuzungumza faida zitokanazo na mafunzo hayo ikiwa ni pamoja na malezi Bora, kuzalisha Mali.
“Kutoa mafunzo ya kuhakikisha wanakuwa Wazalendo, wakakamavu na kuendelea kulinda Taifa letu, na kufanya kazi Ili kuleta Maendeleo kwenye Taifa letu huu ndiyo wakati muafaka” Mhe. Msambatavangu


Hata hivyo amesema kufanya hivyo ndivyo itakavyosaidia vijana hao kutambua uzalendo kwamba wote ni Watanzania kwani ni sehemu isiyoya kibaguzi na kukabila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *