
Leo Mei bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa kiasi cha Shilingi 2,989,967,122,000.00 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 2,767,133,951,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi 222,833,171,000.00 ni kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Ni kufuatia hotuba ya Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo Leo Mei 24 2023 bungeni jijini dodoma.
Baada ya bajeti hiyo kupitishwa na bunge spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Akson kwa mamlaka aliyopewa ametangaza kupitishwa kwa bajeti hiyo ambapo pia ameipongeza Wizara hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulinda amani ya nchi.

Ikumbukwe kuwa Wizara hiyo Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi 87,603,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu, ambapo Fungu 38 – NGOME linatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 22,000,000.00, Fungu 39 – JKT linatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 64,403,000.00 na Fungu 57 – Wizara inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 1,200,000.00.