SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) YAPONGEZWA NA KUPEWA ANGALIZO LA MIKATABA

Kamati ya Kudumu ya bunge ya Maliasili na Ardhi imelipongeza shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa utoaji wa huduma Bora na kulitaka kuhakikisha mikataba ya ubia wanayoingia iwe yenye tija na maslahi mapana kwa Taifa.


Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Thimotheo Mnzava katika kikao kilichojumuisha Wajumbe wa kamati hiyo, shirika la Nyumba la Taifa NHC ambapo piah Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Godfrey Pinda kilichofanyika Leo Mei 23, 2023 katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma huku akieleza umuhimu wa uwepo wa sekta binafsi kutokana na sera waliyonayo.

“Tuwapongeze kwa sera hii, maboresho mliyoyafanya ni makubwa kama ulivyosema mkurugenzi kwenye zama tulizonazo hatuwezi kumtegemea serikali au taasisi za umma zikafanya Kila kitu kikamaliza, tunahitaji sekta binafsi” Mhe. Mzava

“Pamoja na sera hii kujieleza vizuri Bado msisitizo wetu kwenu ni kuendelea kusimamisha maslahi mapana ya taifa, maslahi mapana ya mashirika ya mikataba hiyo mnayokwenda kuyaingia ubia wetu Ili iwe na manufaa kwa Taifa, na mashirika kwa ujumla” Mhe. Mnzava

Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. Godfrey Pinda amesema yote hayo ni matokeo ya mipango ya utekelezaji wa serikali inayoenda kutekelezwa kwa vitendo.

“Tumejipanga kuleta sura mpya ya hizi taasisi ambazo ziko chini yetu na Wizara kwa ujumla” Naibu waziri Pinda.


Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo amepokea pongezi hizo huku akiwahakikishia kufanyia kazi ushauri wa kamati kwa maslahi ya Taifa.

“Wamefurahia uwepo wa sera mpya ya wabia ambayo italeta tija kubwa kwa shirika na kufarijika kuona yale mapungufu yaliyokuwepo kwenye sera ya wabia ya awali tumeyafanyia kazi na tumefanya maboresho makubwa kwenye sera hii mpya”Mhe.Hamad

“Hatua tuliyofikia wabia wetu wanapenda kutayarisha michoro ya kina ambayo itaonyesha thamani yake, angalizo la kamati ni zuri, tumelizingatia na tutaendela kuzingatia hilo” Mhe. Hamad Abdallah Hamad
Ikumbukwe kuwa utekelezaji wa sera ya ubia ya shirika la Nyumba la Taifa huzingatia vigezo na masharti ya ubia katika uendelezaji miliki Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *