WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI YAOMBA KUIDHINISHIWA ZAIDI YA TSH. BILIONI 212 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 212,457,625,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2023/2024.


Ombi hilo limewasilishwa na Waziri wa wizara hiyo Mhe. Nape Mosses Nnauye wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara katika mwaka wa fedha 2023/24 Leo Mei 19, 2023 Bungeni jijini Dodoma.


Aidha kutokana na wasilisho hilo la kuomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 212,457,625,000.00 ni katika michanganuo.


“Kiasi cha Shilingi 30,503,685,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 18,522,155,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 11,981,530,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.Kiasi cha Shilingi 30,503,685,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 18,522,155,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 11,981,530,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.” Waziri Nape
“Kiasi cha Shilingi 181,953,940,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 146,777,440,000.00 ni Fedha za Ndani na Shilingi 35,176,500,000.00 ni Fedha za Nje.” Waziri Nape

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *