
Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe. Mwita Waitara leo Mei 16, 2023 katika kipindi cha maswali na majibu ameiuliza Serikali Bungeni kuwa ni lini itatokomeza matukio ya Mauaji na uporaji wa Mali za Watu katika Wilaya hiyo ambapo takribani Kata Nane Watu wamepigwa Risasi kwa kipindi cha mwezi wa nne hadi Juni 2023
“watu wanapigwa risasi hadharani, na hakuna kilichofanyika, ningeomba nipate Kauli ya Serikali wanachukua hatua gani za dharula ili kurejesha amani katika Jimbo la Tarime na hasa Mji wa Silali ambao ni mji wa mpakani na Biashara imekuwa hai sio nzuri sana” amesema Waitara
Akijibu Swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi. Hamad Masauni amesema hali ya usalama katika Taifa ni nzuri na Serikali inapambana kudhibiti Matukio ya aina yoyote ya uhalifu na hatua zimeshachukuliwa ikiwemo katika Jimbo la Tarime.

Amemhakikishia Mhe. Waitara kama kuna jambo mahsusi na hajaridhika na Hatua zilizochukuliwa amwasilishie Taarifa ili iweze kufanyiwa Kazi.