MBUNGE KISWAGA AISHAURI SERIKALI KUONGEZA TSH. 100 KWENYE MAFUTA.

Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe. Boniventura Kiswaga ameilalamikia serikali kutokupeleka fedha kwenye Wizara ya Kilimo Ili kutekeleza vizuri bajeti yake.

“Kutenga Wizara ya Kilimo inatenga na ipo vizuri sana tatizo hapa nikupewa fedha za utekelezaji wa miradi hii ambayo wameiweka, ndipo tatizo kubwa lilipo” Mhe. Kiswaga

“Tufike mahali tuwe tunaamua haya mambo makubwa haya mambo ya mapinduzi ya Kilimo, Waziri aandae mahindi ya bei nafuu yakauzwe Magu Kuna njaa Kwasababu walilima lakini mvua iliishia Christmas ikapelekea mazao kukauka” Mhe.Kiswaga

Aidha wakati akiendelea kutoa mchango wake amependekeza serikali kuongeza shilingi Mia moja kwenye mafuta huku akieleza tatizo la Watanzania ni kuwa waoga.

“Tuweke tena shilingi miamoja kwenye mafuta, tusiogope tatizo la Watanzania ni kuogopa, tunaogopa wakati wananchi wetu wanakufa masikini, hatuwasaidii Kwasababu tukiongeza shilingi miamoja tukaongeza kwenye mfuko wa umwagiliaji tutafanikiwa kutengeneza skim za umwagiliaji za kutosha” Mhe. Kiswaga

“Inauma sana ili tutekeleze lazima tuwe na mfuko tunaogopa nini? Watanzania ni hawahawa ambao wanahitaji wawe na uchumi endelevu, hawauzi hawazalishi kama ilivyotarajiwa” Mhe. Kiswaga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *