TIMU YA MAWAZIRI WATATU YAWASILI TARIME NA SERENGETI KUTEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU YA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki akiwa ameambatana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula pamoja na Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe. Marry Masanja wamewasili Mkoani Mara kutekeleza Maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu ufumbuzi wa migogoro ya ardhi katika Wilaya za Tarime na Serengeti Mkoani Mara, leo tarehe 06 Mei,2023.

Waziri Mkuu alitoa maelekezo hayo bungeni Dodoma mnamo tarehe 27 Aprili, 2023 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kusimamia masuala ya uhifadhi na namna ambavyo Serikali imekuwa ikizishughulikia.

Waziri Mkuu alielekeza timu ya Mawaziri watatu kwenda kwenye vijiji husika vyenye migogoro katika Wilaya za Tarime na Serengeti kwa lengo la kukutana na Wananchi ili kutoa elimu, ufafanuzi na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo katika vijijiji husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *