WAZIRI KIJAJI ATOA UFAFANUZI SAKATA LA SIMBA CEMENT, TWIGA CEMENT NA CHALINZE CEMENT

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu kijaji ametoa ufafanuzi wa sakata la miradi ya Leganga na Mchuchuma ikiwa ni pamoja na kufata kanuni, taratibu na Sheria na hii ni kufuatia michango ya wabunge mbalimbali bungeni kutaka ufafanuzi wa kina na kauli ya serikali.

Waziri Kijaji ameweka hayo bayana Leo Mei 5 mwaka 2023 wakati akijibu hoja za wabunge bungeni jijini Dodoma na kueleza mikakati ya serikali juu ya Mradi huo huku Moja ya sababu kuu akitaja kuwa ni mwekezaji wa Mradi huo kufilisika.

“Tulipata taarifa rasmi kutoka serikali ya China Mwekezaji yule amefilisika, ni kweli amefilisika lazima tushughulike nayo kwa kufuata kanuni, taratibu na Sheria zetu ili kuliepusha Taifa kuingia katika migogoro ambayo haina maana, aliyefilisika ni yeye lakini bado ana mikataba na sisi” Dkt. Kijaji

“Tulimwita hakuwahi kutokea na sasa tumemuita amekuja yuko mezani, na yeye amekiri kweli amefilisika hivyo ni lazima tuhitimishe naye vizuri ” Dkt. Kijaji

Aidha waziri huyo ametumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi wa kina juu ya Kiwanda cha Chalinze Cement ambacho kilileta kizungumkuti bungeni hapo na kutoa msimamo wa serikali kwa kusema kuwa kama Chalinze Cement anataka kuwekeza nchini wako tayari kumuhudumia.

“Chalinze Cement aje tumsaidie, tunajua yapo mengi yaliyowakwamisha wenzake kama kweli anataka kuwekeza ndani ya Taifa la Tanzania mimi niko tayari waje tuwahudumie” Dkt. kijaji

Tuchukue tahadhari ya hali ya juu na watu wasiolitakia mema nchi yetu, huyu anayekuja kinyumenyume nani? siri yake ni ipi? kwanini asiseme wazi tukajua!”
Mhe. Kijaji

Sanjari na hayo Ameweka wazi suala la kutaka kufanya mazungumzo na Chalinze Cement lakini jitihada ziligonga Mwamba.


“Chalinze Cement nataka kuja kuwatembelea kwenye kiwanda chenu mpaka Leo sijawahi kupata jibu niende au nisiende” Mhe. Kijaji

Ikumbukwe kuwa majibu hayo ya Serikali ni kufuatia hoja za wabunge bungeni na miongoni mwa wabunge waliotaka majibu ya kina na pamoja na Mhe. Ester Bulaya, Joseph Msukuma na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *