SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI KWA KASI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndg: Hamad Abdallah amesema mpaka sasa Shirika hilo linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali kwa Kasi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Ameyasema hayo leo 05 Mei, 2023 Jijini Dodoma, baada ya kutembelea na kukagua miradi ya Mtumba katika eneo la Mji Mkuu wa Kiserikali ambako zinajengwa Ofisi za Wizara mbalimbali na Mradi wa Chamwino.

“Bila shaka ndani ya kipindi cha wiki moja au mbili mtaona kuna Kazi kubwa ambazo zitakuwa zimefanyika saiti, kutakuwa na mabadiliko makubwa” amesema Mkurugenzi Hamad.

Ndg: Hamad amesema kuwa matarajio yao ni kumaliza Kazi ndani ya muda na kwa viwango vizuri huku akisema yeye na Timu yake hawataki kukaa ofisini bali wanatembelea na kujionea maendeleo kwa kila Hatua.

“Mimi saiti nakuja mara kwa mara, toka nimeteuliwa hii ni mara yangu ya nne kuja saiti katika kipindi cha miezi mwili, kwahiyo sikai ofisini napita kwenye kila miradi, sio miradi hii tu ya Mji wa Kiserikali bali na miradi yetu mingine.

Katika hatua nyingine amesema kuwa miradi ambayo alitoa muda ikamilike tayari imekwisha kukamilika ikiwemo Mradi wa Iyumbu ambao wameshauza nyumba kwa baadhi ya wanunuzi.

Pia mradi mwingine ambao unaendelea vizuri ni mradi wa Chamwino ambao umeshauzwa na ametoa muda kuhakikisha unakamilika mwishoni mwa Mwezi Mei, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *