WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA YAOMBA KUIDHINISHIWA ZAIDI YA TSH. 119 BILIONI

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi 119,017,998,000 ikiwa ni Makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.


Maombi hayo Yamewasilishwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na BiasharaMhe.Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb) Wakati akiwasilisha Hotuba Wizara hiyo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2023/24 leo Mei 4, 2023 bungeni jijini Dodoma.


“Katika mwaka 2023/2024, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara inaomba kutengewa jumla ya shilingi 119,017,998,000 katika Fungu 44. Kati ya fedha hizo, shilingi 75,451,494,000 ni matumizi ya kawaida, ambapo shilingi 63,086,267,000 ni mishahara na shilingi 12,365,227,000 ni matumizi mengineyo”Alisema Mhe. Kijaji


“Aidha, shilingi 43,566,504,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo shilingi 30,346,819,000 ni fedha za ndani na shilingi 13,219,685,000 ni fedha za nje” Alisema Mhe. Kijaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *