
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Addallah Ulega amebainisha kuwa Moja ya jukumu kubwa ambalo Wizara itakwenda kutekeleza ni kuyafanya mashamba yaliyotengwa yawe ya uwekezaji, uzalishaji ili yawezekuwa na tija kwa Taifa.
Waziri Ulega ameyasema hayo Leo Mai 3, 2023 wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma.
“Njia ya kwanza ni kwa kutumia fedha zetu wenyewe ambazo tumeziweka kwenye bajeti na kufungua milango ya uwekezaji” Mhe. Waziri
“Wizara ya Mifugo na Uvuvi tumetengeneza mpango ambao siyo wa kutegemea mvua tena, tunaenda kumwagilia” Mhe Waziri Ulega.
“Msiwe na wasiwasi wowote sisi ni watu wasikivu na ni watu ambao tukotayari kushirikiana nanyi ipasavyo” Mhe. Waziri

Aidha amezungumzia Swala la Watanzania kutumia fursa ya uzalishaji Malisho hapa nchini kwasasa kwani hiyo ni fursa ya kupata fedha za kigeni na kupunguza changamoto ya ajira kwani njia rahisi ya kuinua ni katika Mifugo huku akiwaahidi wabunge kuchukua Michango yao ya kimawazo na kufanyia utatuzi changamoto zinazowakumba wavuvi.
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi Shilingi 295,920,933,000.00 ikiwa ni Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka 2023/2024.