WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAOMBA ZAIDI YA TSH. BILIONI 2095 KWAMWAKA WA FEDHA 2023/24

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeomba kuidhinishiwa kiasi cha Shilingi Shilingi 295,920,933,000.00 ikiwa ni Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo katika mwaka 2023/2024.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara hiyo leo May 2, 2023.


“Katika mwaka 2023/2024, Wizara inaomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya jumla ya Shilingi 295,920,933,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 112,046,777,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mifugo (Fungu 99) na Shilingi 183,874,156,000.00 kwa ajili ya Sekta ya Uvuvi (Fungu 64). Mchanganuo wa fedha zinazoombwa kwa kila Fungu ni kama ifuatavyo” Alisema Mhe. Ulega


“Wizara inaomba kutumia jumla ya Shilingi 112,046,777,000 kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Sekta ya Mifugo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 50,122,670,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 61,924,107,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo” Alisema Mhe. Ulega


Mgawanyo wake ukiwa ni Fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 50,122,670,000, Mishahara Shilingi 23,939,807,000, Matumizi Mengineyo (OC) Shilingi 26,182,863,000, Fedha za Matumizi ya Maendeleo Shilingi 61,924,107,000, Fedha za Ndani, Shilingi 56,592,173,000, Fedha za Nje, Shilingi 5,331,934,000.


Aidha katika Sekta ya Uvuvi Wizara imeomba jumla ya Shilingi 183,874,156,000 kwa ajili ya kutekeleza majukumu katika mwaka 2023/2024 ambapo Kati ya fedha hizo, Shilingi Shilingi 49,462,296,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 134,411,860,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.


“Mchanganuo wake ukiwa ni Fedha za Matumizi ya Kawaida: Shilingi 49,462,296,000, Mishahara ni Shilingi 15,368,951,000, Matumizi Mengineyo (OC) ni Shilingi 34,093,345,000, Fedha za Matumizi ya Maendeleo Shilingi 134,411,860,000, Fedha za NdaniShilingi 110,682,025,000, Fedha za Nje Shilingi 23,729,835,000” Alisema Mhe. Ulega

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *