WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ILIVYOJIPAMBANUA KWENYE RASIRIMALI MALISHO, VYAKULA NA MAJI KWA MIFUGO

Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) imeendelea kuimarisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo ambapo bwawa la Kimambi (Liwale) lenye ujazo wa lita milioni 95 na Matekwe (Nachingwea) lenye ujazo wa lita millioni 102 yamejengwa, na bwawa moja (1) la Mhanga (Itigi) lenye ujazo wa lita Milioni 54 limekarabatiwa.


Hayo yamemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2023/2024 leo May 2, 2023 bungeni jijini Dodoma.
Mhe. Ulega amesema Wizara imekamilisha ujenzi wa kisima kirefu cha Lwami katika Wilaya ya Mwanga na kuendelea na ujenzi wa mabwawa 11 na visima virefu vitatu katika Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini.


“Wizara kwa kushirikiana na ORTAMISEMI imetambua na kuyasajili maeneo 77 ya malisho yenye jumla ya hekta 994,827.29 kutoka kwenye Halmashauri 8 za Wilaya za Mwanga, Tanganyika, Mvomero, Kiteto, Mbulu, Simanjiro, Longido na Karatu” Alisema Mhe. Ulega


“Ili kuongeza upatikanaji wa malisho na mbegu za malisho, katika mwaka 2022/2023 mashamba mawili (2) ya kuzalisha mbegu za malisho na malisho yameimarishwa kwa kuyapatia vitendea kazi vikiwemo hay bailer mbili, hay rake mbili na mower tatu pia mashamba ya Wizara na taasisi zake yamezalisha mbegu bora za malisho kilo 22,691.65 ikilinganishwa na mwaka 2021/2022 ambapo uzalishaji ulikuwa jumla ya kilo 4,481.90” Alisema Mhe. Ulega


Aidha amesema lengo la Mpango huo ni kuwafundisha kwa vitendo wafugaji namna ya kulima, kupanda, kutunza, kuvuna na kuhifadhi malisho na mbegu.


“Viwanda vipya 22 vya kuzalisha vyakula vya mifugo vimesajiliwa katika Mikoa 8 ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Mbeya, Pwani na Shinyanga na kufanya viwanda vya kuzalisha vyakula vya mifugo kuongezeka kutoka 199 mwaka 2021/2022 hadi 221 mwaka 2022/2023″Alisema Mhe. Ulega


Hata hivyo ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuboresha ubora na usalama wa vyakula vya mifugo, Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa imetoa mafunzo kuhusu mfumo wa Utoaji wa Vibali vya Kielektroniki (MIMIS) kwa wakaguzi 212 wa rasilimali za vyakula vya Mifugo katika mikoa 26 nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *