TAMISEMI SPORTS CLUB YANG’ARA MCHEZO WA DRAFTI, FOOTBAL NA RIADHA

Timu ya Tamisemi Sports Club imeng’ara katika mashindano ya Mei Mosi baada kuibuka washindi katika mchezo wa draft kushinda nafasi ya kwanza, mpira wa miguu nafasi ya pili na kwa upande wa riadha wanawake kushinda nafasi ya pili.

Haya yamejidhihirisha leo kwa timu hiyo baada ya kuwasili kutoka Mkoani Morogoro ambapo mashindano hayo yalikua yakifanyika na kukabidhi makombe ya ushindi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bw.Adolf Ndunguru katika ofisi za Sokoine Jijini Dodoma.

Bw. Ndunguru aliwapongeza timu hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri katika michezo na kuwataka michezo hiyo kuendelezwa na sio tu kwa ajili ya kutafuta ushindi bali aliwaambia mchezo pia husaidia afya, umoja na kuleta mahusiano mazuri katika kazi.

Amesema kuibuka kwa ushindi huo kunaendelea kuwapa moyo viongozi pamoja na watumishi wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuendelea kuisapoti timu hiyo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Tamisemi Sports Club
Lwitiko Mwasege ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na uongozi wa timu kwa kuendelea kuwajali na kuhakikisha timu inakua imara na kuahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *