
Huko kwenye mazao ya bahari Kuna fedha nyingi ambazo serikali inazipoteza, Kuna fursa nyingi ambazo serikali ingeweza kuwekeza kupunguza changamoto yaukosefu wa ajira kwasababu watu wamehamasika wanatamani wafanye, wanachoshindwa ni uwezeshwaji.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe. Tunza Malapo wakati akitoa mchango wa hotuba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega aliyoiwasilisha leo May 2, 2023 bungeni jijini Dodoma.
Mheshimiwa Malapo amebainisha kuwa wananchi wamehamasika kufuga viumbe wa majini lakini changamoto inayowakumba ni swala la uwezeshwaji pamoja na ufuatiliaji wa serikali.

“Mheshimiwa ulienda kuzindua hivi yangu umezindua umewahi kuwauliza wanaendeleaje? hivyo vifaranga vya majongoo havijapatikana na hawajui hatima yao kumbuka wale watu wamewekeza fedha zao wameweka vizimba vizuri, wanalipa walinzi Majongoo vifaranga vitoke Bagamoyo vikifika mtwara vimekufa lakini mnawaambia wasubiri watakuja watakuja lini?” Alisema Mhe. Ulega
“Serikali haijaona umuhimu wa sekta ya Uvuvi? Serikali ilisema itanunua maboti 158 igawe kwa wavuvi lakini kule Manispaa ya Mtwara mpaka sasa hivi wako kwenye michakato tu, hakuna boti lililofika na wakiwa kwenye michakato mingine Ile ya mwanzo haijatekelezwa kwanini tunafanyiwa hivi kwenye sekta hii?” Alisema Mhe. Malapo
Hata hivyo amehitimisha kwa kuiomba serikali kukamilisha michakato ya boti na kuwapatia wavuvi kuendeleza kazi zao za Uvuvi ikiwemo kutumia wataalamu waliopo kwenye sekta hiyo.