KAMPUNI YA ASAS YAPONGEZWA KWA KAZI NZURI

Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles John Poul Mwijage ametoa pongezi kwa kampuni ya uzalishaji wa maziwa hapa nchini ASAS kwa kazi nzuri huku akiwataka wananchi wanaokopeshwa Ng’ombe na Kampuni hiyo wafanye kulingana na makubaliano.

Mbunge huyo amesema hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa mapema leo May 2 2023 na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Abdallah Ulega Bungeni jijini Dodoma.

“Nitoe pongezi kwa kampuni ya maziwa ya ASAS Kazi mliyoifanya ya Ujombani, Rungwe ni nzuri, kampuni ya ASAS inaagiza Ng’ombe wa maziwa kutoka Afrika Kusini na Ng’ombe mmoja ukimlisha unapata kilo 25, anawakopesha watu wanafuga halafu hamumrudishii” Mhe Mwijage

Leta Asas Company Limited tumpe ardhi awagawie wananchi wa Kagera ajenge viwanda, watu waelewe hekta Laki sita za NARCO nusu yake iko Kagera
Ametumia nafasi hiyo kuunga mkono hoja kwa mujibu wa hotuba iliyotolewa huku akiitaka serikali kuwekeza zaidi kwenye Wizara hiyo kwani ni miongoni mwa Wizara zinazozalisha fedha kwaajili ya pato la Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *