WATUMISHI TAMISEMI WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKUKUU YA MEI MOSI

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wameshiriki maadhimisho siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1 Mei ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro huku kaulimbiu ikiwa “Mshahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi”

Awali akisoma hotuba yake Naibu Waziri, Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amewataka waajiri kushirikiana na vyama vya wafanyakazi wakati wa kuanzisha vyama hivyo ili vianzishwe kwa mujibu wa Sheria.

Mhe. Sagini amewataka waajiri hao pia kutokwepa kuanzisha vyama vya wafanyakazi sehemu za kazi kwa kuwa vipo kisheria.

“Lakini kwa maandamano haya hapa Dodoma na waajiri kuwaruhusu wafanyakazi kuja hapa katika maandamano na kugharamia mapambo ni dalili njema ya kuwa waajiri sio wakorofi” amesema Mhe. Sagini

Jumla ya watumishi 26 wamechaguliwa kuwa wafanyakazi hodari kwa mwaka 2023 ambapo kila Idara na vitengo ilitoa mwakilishi.

Aidha, Bw. Fulgence Matemele Mchumi kutoka Idara ya Serikali za Mitaa (DLG) alichaguliwa kuwa mfanyakazi hodari wa Wizara kwa mwaka 2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *