DKT. BITEKO AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI ZA MADINI MOROGORO, MAHENGE

Ataka kasi ya ubunifu, uzalendo kuongezeka kwenye utendaji kazi

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amekutana na wafanyakazi wa Tume ya Madini kutoka Ofisi za Maafisa Madini Wakazi za Mikoa ya Kimadini ya Morogoro na Mahenge na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango kwenye Pato la Taifa.

Waziri Biteko ameyasema hayo leo kwenye kikao chake na watumishi wa ofisi husika mkoani Morogoro mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kitaifa katika mkoa wa Morogoro.

“Hongereni sana kwa kuendelea kuipaisha Sekta ya Madini kupitia uchapakazi wenu makini, tunataka kuhakikisha mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025, mimi pamoja na timu ya Wizara ya Madini tutaendelea kuweka mazingira mazuri ya kazi huku tukitatua changamoto mbalimbali,” amesema Waziri Biteko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *