
Ili kupandisha hadhi shule ni kujenga miundombinu ambayo inatakiwa, halafu kuiombea usajili kutoka Wizara ya Elimu. Mhe Ndejembi
Kauli hiyo imetolewa Leo April 28, 2023 bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. Charles Kimei
Kwakuwa kata ya Mamba Kaskazini na Kusini Kuna shule nyingi za sekondari lakin hakuna shule hata moja ya kidato cha tano na Sita Je? Serikali ipo tayari kuipandisha hadhi shule ya Mboni Sekondari na kuijengea Hosteli? Mhe. Kimei

“Tutakaa na Mheshimiwa Mbunge kuona shule hizi kama miundombinu inakidhi vigezo, na kama inakidhi vigezo tuone utaratibu wa kuziombea usajili wa kuweza kupata mkondo wa kidato cha tano na Sita. Mhe. Ndejembi