WIZARA YA MADINI YAOMBA ZAIDI YA SHILINGI BILION 89, MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeomba kuidhinishiwa kiasi cha 89,357,491,000.00 (Bilioni themanini na tisa Milioni miatatu hamsini na saba, mia nne tisini na moja Elfu) kwaajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Ombi hilo limewasilishwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Mashaka Biteko wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 leo April 27, 2023 bungeni jijini Dodoma.

“Ili Wizara iweze kutekeleza majukumu na malengo yaliyopangwa ikiwemo ukusanyaji wa maduhuli ya shilingi 1,006,705,169,300.00, naomba Bunge lako Tukufu liridhie na kupitisha makadirio ya shilingi
89,357,491,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024″ Dkt. Biteko


“Shilingi 23,172,550,000.00 ikiwa ni fedha za maendeleo na Shilingi 66,184,941,000.00 kwa ajili ya
Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi 20,307,498,000.00 ni kwa ajili ya
Mishahara na shilingi 45,877,443,000.00 ni Matumizi Mengineyo” Dkt. Biteko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *