KAMATI YA MAWAZIRI NANE KWENDA TARIME, BUNDA NA SERENGETI

Serikali imeiagiza Kamati ya Mawaziri nane kwenda kufanya mazungumzo na Wananchi wa Tarime vijijini, Serengeti na Bunda kwani ndiyo mahitaji yao makubwa ili watambue kikamilifu Mipaka yao iko wapi ili wapate fursa ya kuwasilisha hoja na mahitaji yao ili Serikali ifanyie kazi.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa Kauli hiyo Leo April 27, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Mwita Waitara lililokuwa likihitaji Mawaziri nane kwenda kwenye jimbo la Tarime Vijijini kwa kutoa elimu pamoja na kusikilia kero na changamoto zao.

“Wasaidie wananchi wa Tarime vijijini, Serengeti na Bunda ni lini hao Mawaziri wataenda kuwasikiliza hao wananchi wale ili kutoa elimu na kutambua” Mhe. Mwita Waitara


“Kuanzia tarehe 2 May 2023, baada ya sherehe za Mei Mosi, ninauhakika kati ya tarehe 3 na nne watakuwa tarime” Mhe. Majaliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *