KITABU CHA MCHAKATO WA KUWA MIMI KUZINDULIWA RASMI JIJINI DODOMA.

Na; Emmanuel Charles.


Kama ilivyo kwa Binadamu kutakiwa kujifunza na kupata maarifa juu ya jambo fulani, hivyo hutumia njia mbalimbali ili kupata maarifa hayo.

Mojawapo ya njia Bora inayoaminika na inayoweza kukupa maarifa ni kusoma Vitabu
Kupitia vitabu watu hujifunza na kupata maarifa juu ya mambo fulani.
Kuhusiana na hilo, Pastor Raphael Lyela wa Dodoma, yeye ameamua kuandaa Simulizi ndefu ya maisha yake ambayo kwa kiasi kikubwa itakupa funzo.

Simulizi hii ameiandaa kupitia kitabu chake ambacho kwa mjibu wake anasema kuwa amekiandaa kwa mfumo wa nyakati, ambapo Simulizi hiyo itakuwa na Kitabu cha kwanza kinachoitwa MCHAKATO WA KUWA MIMI, kisha KUWA MIMI na baadae MIMI.
Kwa sasa amekwisha kufanikiwa kuandaa Kitabu cha MCHAKATO WA KUWA MIMI ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa mnamo Siku ya Tarehe 07 Mei, 2023 Jijini Dodoma.
Pastor Lyela amezungumza na wanahabari Jijini Dodoma na kuwaeleza kwa ufupi kuhusu Kitabu hicho.


amesema Sababu za kuandaa Kitabu hicho ni pamoja na kuwa Tatizo la watu wengi hawapendi mchakato na kupenda Matokeo.
“wanapenda kuviona vitu vikiwa na matunda bila kujali vimefikaje hapo, na hata asilimia kubwa kwa vijana ambao wanapenda mafanikio ambayo hayana utaratibu au yenye utaratibu wa njia fupi(Shortcut) ambao sio wa kuvumilia” amesema Mch. Raphael
Anasema mpaka kufika hapo alipo ilikuwa ni mchakato ambao ulikuwa na Uvumilivu, na kusamehe.


ameeleza kuwa ukivumilia mchakato utapata matunda ambayo yatadumu kwa sababu yalipitia mchakato unaostahili.
Sababu nyingine ni, kuonyesha kwamba mchakato sio jambo la hasara na kusubiri inahitaji nguvu.

Sababu nyingine amesema, ni kufundisha jamii Kanuni
“ukimfundisha mtu Kanuni anaweza kufanikiwa bila kujali mahali alipo, mimi nimeona mpaka hapa nilipo kuna Kanuni ambazo zimenisaidia ambazo ninaamini mtu mwingine akijifunza kupitia Kanuni pia inaweza kumsaidia.
Sababu nyingine Mchungaji amesema ni kuongeza nguvu ya ushawishi kwa watu ambao anaweza kuwafikia kupitia Kitabu, licha ya kwamba amekuwa akifundisha kwa njia mbalimbali, lakini Kitabu ni njia mojawapo ambayo ushawishi wake unaweza kuongezeka na watu wakapata Kumbukumbu ya kudumu kwa vizazi na vizazi.

Kwa upande mwingine amegusia aina ya Maudhui yanayopatikana kwenye Kitabu hicho ambayo ni
Historia ya Maisha yake, ambapo kupitia Historia hiyo watu wataguswa na itagusa maisha ya watu.
Akizungumzia kuhusu eneo la Maadili katika Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla amesema mojawapo ya maudhui yanaeleza kuhusu changamoto za vitendo vya jinsia moja ambapo ameeleza namna ya kushinda changamoto hizo.

“ukimfundisha mtu Kanuni akaielewa inaweza kumsaidia kushinda hizo changamoto, naamini mtu ambaye atapata kukisoma hicho Kitabu itamsaidia namna ya kuweza kuzishinda.”ameeleza Mch. Rafael.

Kuhusu Changamoto alizokutana nazo wakati wa kukiandaa Kitabu hicho ni kuugawanya muda, kwa sababu unakuwa na mambo mengi unafanya na kutakiwa kupata muda wa kupanga, hivyo kuna Vijana ambao ameshirikiana nao katika mchakato wa kukiandaa.

Katika Hatua nyingine alipoulizwa Swali na Mwanahabari kuhusu Wazo la kukiandaa Kitabu kinachomhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alijibu kwa kusema yupo tayari kukiandaa iwapo ataruhusiwa na Mamlaka.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uzinduzi wa Kitabu Eng. Adam Sebastian amesema hafla hiyo itafanyika katika ukumbi wa Mabeyo Jijini Dodoma na unatarajiwa kukutanisha wadau mbalimbali wa Kitaifa na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Antony Mavunde.
Mwisho, watu wote wamekaribishwa katika Hafla hiyo ambayo hakutakuwa na Kiingilio chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *