DC BOMBOKO AZINDUA ZOEZI LA CHANJO UKEREWE

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Hassan Bomboko amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawapeleka kupata chanjo watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na mabinti wenye umri chini ya miaka 14 ambao bado hawajavunja ungo ili kuwakinga na saratani ya shingo ya kizazi

Bomboko amesema zoezi la utoaji wa chanjo hiyo litadumu kwa muda wa mwezi mmoja huku Watoto wadogo wakipewa kwenye zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali ya wilaya na mabinti wenye umri chini ya miaka 14 wakifuatwa kwenye shule wanazosoma

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ya Ukerewe amewatoa hofu wazazi kuhusu chanjo hiyo na kusema inakinga magonjwa takribani 14 na kwamba mtoto au binti atakayeipata chanjo hiyo atakuwa amejikinga na magonjwa hayo na hivyo kumuwezesha kuishi salama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *