NEEMA KUBWA YAWAFIKIA WAKAZI WA CHAMWINO JIJINI DODOMA

Kuelekea sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amezindua mradi wa ujenzi wa tenki la kuhifadhi majisafi lenye ujazo wa lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Jijini Dodoma.

Mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 1.6 badala ya 2.5 utawezesha kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 42 mpaka 87 katika wilaya ya Chamwino.

E90A2334.JPG

Akizungumza leo Aprili 25, Wilayani Chamwino wakati wa uzinduzi wa Mradi huo Mhe.Senyamule,amesema kuwa maandalizi ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa mkoa wa Dodoma unaendelea kwa kuzindua miradi mbalimbali ukiwemo huo wa maji.

“Niwapongeze watumishi na uongozi wote wa DUWASA mkiongozwa na Mhandisi Aron Joseph, kwa ubunifu huu wa kuokoa pesa nyingi za serikali kwa kubuni namna nzuri ya usimamizi wa ununuzi wa vifaa na kumkabidhi Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na yeye kutekeleza mradi huu kwa uaminifu mkubwa ukweli ni kwamba mmefanya kazi nzuri,”amesema Senyamule

E90A2290.JPG

Mkuu huyo wa mkoa amesema Muungano umebaki kama kielelezo kwani ni miongoni mwa Muungano uliodumu na umekuwa na faida kubwa katika nchi hizi hasa katika sekta za Maendeleo.

Pia ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo ndio inayohusika na Muungano kwa kuendelea kuondoa kero za Muungano na kuendelea kuboresha na kuufanya kuwa imara na kuvutia mataifa mengine ambapo wanaendelea kujiuliza siri ni nini ya Muungano huo kudumu kwa miaka mingi.

E90A2284.JPG

“Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano ambayo yanafanyika kila mwaka tarehe 26,Aprili sisi tumeamua kama mkoa wa Dodoma kuzindua mradi huu mkubwa wa maji safi katika wilaya hii ya Chamwino ambayo ni wilaya ya kimkakati katika harakati za Serikali kuhamia Dodoma,”amesema Senyamule 

Senyamule amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa vyanzo vya maji ,kutunza maji na kuhakikisha wanalipa bili za maji ili kufanya mradi uwe endelevu.

E90A2269.JPG

Pia Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wawekezaji wote wanaotakakuwekeza Chamwino kuja kuwekeza kwani kuna uhakika wa upatikanaji wa maji hivyo ni eneo salama kwa uwekezaji.

”Kila mwekezaji ambaye alikuwa anataka kuja kuwekeza Chamwino kitu cha kwanza alikuwa akiulizia Maji akiambiwa hakuna anakata tamaa kwa sasa maji yamekuja wenye nia ya kuwekeza Chamwino Njooni Neema ya Maji imekuja Chamwino”amesema Senyamule.

E90A2309.JPG

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema Kitaifa upatikanaji wa maji umefikia 37% na asilimia 88% wanapata maji kwa mjini.

Kemikimba ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa kwa Mkoa wa Dodoma ni uchimbaji wa Visima maeneo ya pembezoni ambapo Bilioni 4.8 zitatumika eneo la Nzuguni kuchimba visima ambapo utazalisha maji lita milioni 7 kwa siku na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka 2023.

E90A2288.JPG

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa Mradi mkubwa wa miji 28 Chamwino ikiwepo unaendelea na mkandarasi anaendelea na ukikamilika kutakuwa na uhakika wa kupunguza changamoto ya maji.

Mhandisi Kemikimba amenainisha kuwa ,Ili kuhakikisha matatizo ya maji yanapungua Jijini Dodoma serikali imeanza kufanya utafiti wa kutoa maji kutoka Bwawa la Mtera na Bwawa la Farkwa na kwa upande wa Bwawa la Farkwa tayari utaratibu wa kuwalipa wananchi Fidia ya bilioni 7 ambapo mradi huo ukikamilika utazalisha maji lita milioni 120 kwa siku.

E90A2461.JPG

Pia amebainisha Mpango mwingine ni kutoa maji ziwa Victoria ambapo hayo ndio yatakuwa maji ya uhakika na kama ilivyo kawaida Bomba linapopita eneo haliwezi kupita bila kuhudumia wananchi wa eneo linapopita hivyo hata Mkoa wa Singida utanuafaika.

Amezungumzia pia Malengo ya kimataifa ambapo Wizara ya maji inaendelea kutimiza Malengo hayo ya kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.

E90A2520.JPG

Naibu Katibu Muungano Abdalhassan Mitawi amesema kuwa Mwaka huu wamekuja tofauti katika sherehe hizo za Muungano na utofauti huo utasaidia kupeleka sherehe hizo kwa wenye Muungano wao kwa maana ya kuupeleka kwa wananchi kwani wao ndio wanaoumiliki na sherehe hizo zinakwenda sambamba na uzinduzi wa Miradi mbalimbali katika jamii.

E90A2355.JPG

Hata hivyo baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chamwino wametoa shukrani Kwa Rais Samia pamoja na Mamlaka ya Maji Mkoani Dodoma kwa kuzindua kisima hicho kutokana na adha walizokuwa wanakumbana nazo huku wakisema mradi huo umeleta neema wilayani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *