
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Imeomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi 14,731,640,000.00 Fungu namba 26 la Makamu wa Rais, ikiwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida kwa mwaka 2023/24, na shilingi 39,370,444,000.00 kwa ajili ya Fungu 31 la Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni Makadirio ya Matumizi kwa mwaka 2023/2024.
Hotuba hiyo imewasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo kuhusu Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2023/2024 leo April 24, 2023 bungeni jijini Dodoma.
“Ninaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe Makadirio ya Matumizi ya Shilingi 14,731,640,000.00 Fungu namba 26 la Makamu wa Rais, ikiwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida kwa mwaka 2023/24. Kati ya kiasi hicho, Shilingi 1,251,640,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya watumishi na Shilingi 13,480,000,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.” Alisema Waziri Jafo
“Ninaomba Bunge lako Tukufu, liidhinishe makadirio ya Matumizi ya Shilingi 39,370,444,000.00 kwa ajili ya Fungu 31 kwa ajili ya Fungu 31 la Ofisi ya Makamu wa Rais, Kati ya kiasi hicho, Shilingi 20,712,399,000.00 ni kwa ajili Matumizi ya Kawaida na Shilingi 18,658,045,000.00 ni Matumizi ya Miradi ya Maendeleo.” Alisema Waziri Jafo
“Matumizi ya Kawaida yanajumuisha Shilingi 3,349,788,000.00 Mishahara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Shilingi 5,264,448,000.00 Mishahara ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na Shilingi 12,098,163,000.00 Matumizi Mengineyo. Aidha Matumizi ya Miradi ya Maendeleo yanajumuisha Shilingi 3,602,000,000.00 fedha za Ndani na Shilingi 15,056,045,000.00 fedha za Nje.” Alisema Waziri Jafo