BONDIA HASSAN MWAKINYO AMBURUZA KUVESA KATEMBO

Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo ashinda pambano la kirafiki dhidi ya mtani wake Kuvesa Katembo raia wa Afrika Kusini

Pambano hilo la (pambano la main card) la raundi nane (8) lililomkutanisha bondia mtanzania Hassan Mwakinyo akichuana na bondia kutoka nchini Afrika Kusini Kuvesa Katembo lililofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Leo usiku April 24, 2023 jijini Dodoma, lililobeba dhima ya kuchangia taulo za kike kwa watoto wa kike katika Mikoa ya Nyanda za juu kusini lililandaliwa na mbunge wa Viti Maalum Sophia Maajagenda kupitia Lady in Red promotion.

Raundi hizo nane zimetoa matokeo ya Kumtangaza Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo kuwa mshindi wa pambano hilo dhidi ya mpinzani wake Kuvesa Katembo waliopishana kwa alama chache.

Akizungumza mara baada ya shindano hilo lililokuwa la ushindani bondia Hassan Mwakinyo ameisisitiza jamii kuendelea kupinga ukatili katika jamii inayowazunguka.

Katika pambano hilo la ngumi Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana amempongeza bondia huyo kwa ushindi alioupata kwani ameipeperusha bendera ya Taifa kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *