JESHI LA POLISI LAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL-FITR

Na Tamimu Mbegu – Polisi makao makuu -Dodoma


Katika kuelekea sikukuu ya Eid el-fitr, Jeshi la Polisi nchini limesema hali ya
usalama ni shwari na kwamba litaendelea kusisitiza jamii kuendelea kushirikiana
na Polisi katika kubaini na kuzuia uhalifu hususani unaotokana na mmomonyoko
wa maadili unaoiandama dunia kwa sasa pamoja na ajali za barabarani
zinazosababisha vifo na majeruhi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tahadhari kuelekea sikukuu hiyo,
April 20, 2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime alisema kuwa waumini wa dini
ya kiislamu wiki hii watahitimisha ibada muhimu katika uislamu ya mfungo wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani na sote kwa pamoja tutasheherekea sikukuu ya Eid
el fitr kwa kushiriki ibada na baada ya ibada waumini na wasiowaumini pia
watasheherekea katika maeneo mbalimbali baada ya baraza la Eid.
SACP Misime alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini limejipanga kikamilifu kwa
kushirikiana na viongozi wa dini ya kiislamu na wananchi kuhakikisha usalama
unaimarishwa maeneo yote ili kutoa fursa ya kusheherekea kwa amani na utulifu,
makamanda wa mikoa na vikosi watasimamia usalama kulingana na mazingira na
mikoa na vikosi vyao.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda
watotoili wasipatwe na madhara ya aina yoyote wanapokuwa wakisheherekea
sikukuu katika maeneo mbalimbali.
Sikukuu ya Eid el- fitr inatarajiwa kusheherekewa kesho au kesho kutwa
kuloingana na muandamo wa mwezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *