
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya TaTEDO-SESO ambao ni watengenezaji wa bidhaa zinazotumia umeme kwa gharama nafuu.

Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 19, 2023 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamemuelezea na kumuonesha Mhe. Spika ubora wa bidhaa zao.
