
Imebainishwa kuwa Sheria za Tanzania haziruhusu Mahusiano ya jinsia moja kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria ya Ndoa na kwa mujibu wa kifungu 154 sura ya 16 cha sheria y kanuni ya adhabu kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ya jinsia ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifungo cha maisha jela au kifungo kisichopungua miaka 30 jela.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul wakati akijibu swali la Mbunge wa viti Maalum Mhe.Anatropia Lwehikila Alilouliza Je? Sheria za Tanzania zinasema nini kuhusu mahusiano ya jinsia moja.
Kufuatia majibu hayo ya Naibu Waziri Mbunge huyo akasimama kwa swali la nyongeza la kutaka kujua kwakuwa sheria ziko wazi kupinga mapenzi ya jinsia moja, Serikali imechukua hatua gani kwa wahanga wanaojinasibu kwa vitendo hivyo kwenye Vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua, kuwapeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria?

“Je ni lini Serikali italeta lini mabadiliko ya sheria ili kila anayejihusisha aweze kuchukuliwa hatua lakini piah tuweze kulinda maadili ya nchi yetu?”
Naibu Waziri Gekul akabainisha hatua zimekuwa zikichukzilizochukuliwa huku akitoa rai kwa jamii kuchukua tahadhari lakini piah mahakama zimekuwa zikitoa hukumu na endapo utafiti wa kina ukishakamilika kuwepo kwa kauli ya pamoja na serikali ipo tayari.

Kufuatia hilo likamuibua Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Mhe. Nape Nnauye ambapo amesema miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na serikali katika sekta yake tayari wameshavifungia Baadhi ya vyombo vya habari Vya Mtandaoni ambavyo vilikuwa vinarusha matangazo hayo na mpaka hivi sasa hakuna matangazo ya mapenzi ya jinsia moja kwenye Vyombo vya Habari.