TAMISEMI ILIVYOJIPAMBANUA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII

Ili kuimarisha huduma za Ustawi wa Jamii kwa makundi maalum, hadi Februari, 2023 Ofisi ya Rais Tamisemi imefanikiwa kuwatambua jumla ya Watu Wenye Ulemavu 10,035 ambapo Wanawake ni 6,100 na Wanaume 3,935.
Hayo yameemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angela Kairuki wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha wa 2023/2024 leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri Kairuki amesema Miongoni mwa Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi 2,400 kati yao Wanawake ni 1,300 na Wanaume 1,100; Watu Wenye Ulemavu wa Viungo 5,233 ambapo Wanawake ni 3,133 na Wanaume 2,100; Wasioona 510 ambapo Wanawake ni 203 na 24 Wanaume 307; Viziwi 1,500 kati yake Wanawake ni 785 Wanaume 715; na Watu Wenye Ulemavu wa Akili 392 ambapo Wanawake ni 281 Wanaume 111.42.
“Watu hao Wenye Ulemavu wametambuliwa na kupewa Vifaa saidizi ikiwemo miwani 754, miamvuli 934, mafuta ya Ngozi 1,741, fimbo nyeupe 306, kofia 915, na baiskeli za miguu mitatu 293 ili kuwawezesha kujimudu” Alisema Waziri Kairuki
Aidha amebainisha Kuundwa kwa Kamati 5,024 za Watu Wenye Ulemavu katikaVijiji na Kamati 2,284 katika Mitaa. Kamati hizo zinahusisha wajumbe mchanganyiko (Watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu).
“Lengo la Kamati hizo ni kusimamia masuala ya watu wenye ulemavu na kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili ikiwepo mawasiliano ya lugha ya alama, jumla ya wazee 2,117,637 wametambuliwa katika Mikoa 26, kati ya wazee hao wanawake ni 735,169 na wanaume ni 1,382,468. Kati yao wazee 585,672 sawa na asilimia 27.65 wamepatiwa vitambulisho vya Bima ya afya kwa ajili ya matibabu ambapo wanawake 330,176 na wanaume 255,496.” Alisema Waziri Kairuki


Katika swala la wazee yameundwa Mabaraza ya ushauri ya wazee 20,748 kwenye Mikoa/Halmashauri na Ngazi ya Kata, Vijiji/Mitaa kwa ajili ya usimamizi ya masuala ya wazee sambamba na madirisha 588 ya kutolea huduma za Afya ya Msingi kwa wazee yameanzishwa katika 25 Hospitali za Halmashauri, vituo vya afya na zahanati.
Aidha Halmashauri kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe inatoa huduma kwenye vituo jumuishi (One stop Center) ambapo hadi sasa kuna vituo 16 katika Halmashauri za Majiji ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam, Halmashauri za Manispaa za Tabora, Kinondoni, Kigoma, Shinyanga, Iringa, Kahama na Halmashauri za Wilaya za Msalala, Kasulu, Ikungi, Kibaha, Hai na Mvomero.
“Halmashauri zimeweza kushughulikia masuala ya Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Hadi Februari, 2023 watoto 335,971 wametambuliwa na kati yao watoto wa kike ni 167,337 na watoto 168,634 ni wa kiume” Alisema Waziri Kairuki
Hata hivyo watoto hao wameweza kupatiwa misaada mbalimbali ikiwemo chakula, malazi, mavazi, elimu, matibabu na watoto 26,000 waliunganishwa na familia zao na kuhakikisha watoto hao wanaishi kwa amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *