
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Trilioni Tisa Bilioni Mia Moja Arobaini na Nne Milioni Ishirini na Moja na Mia Sita Tisini na Tisa Elfu (Shilingi 9,144,021,699,000) kwa ajili ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI Fungu Namba 56, Tume ya Utumishi wa Walimu, Fungu Namba 2 na Mafungu 26 ya Mikoa yanayojumuisha Halmashauri 184 ikiwa ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2023/24.
Ombi Hilo limewasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angela Kairuki wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 leo April 14, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.
“Kati ya fedha zinazoombwa, Shilingi Trilioni Tano Bilioni Mia Sita Hamsini na Nane Milioni Ishirini na Mbili na Hamsini na Nane Elfu (Shilingi 5,658,022,058,000) ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida yanayojumuisha Mishahara Shilingi Trilioni Nne Bilioni Mia Tano Tisini na Saba Milioni Mia Sita Thelathini na Mbili na Mia Moja Themanini na Tatu Elfu (Shilingi 4,597,632,183,000) na Matumizi Mengineyo Shilingi Trilioni Moja Bilioni Sitini Milioni Mia Tatu Themanini na Tisa na Mia Nane Sabini na Tano Elfu (Shilingi 1,060,389,875,000)” Alisema Waziri Kairuki

“Jumla ya Shilingi Trilioni Tatu Bilioni Mia Nne Themanini na Tano Milioni Mia Tisa Tisini na Tisa na Mia Sita Arobaini na Moja Elfu (Shilingi 3,485,999,641,000) zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Trilioni Mbili Bilioni Mia Tatu Sitini na Mbili Milioni Mia Saba na Mia Nne Themanini na Saba Elfu (Shilingi 2,362,700,487,000) ni fedha za ndani” Alisema Waziri Kairuki.
“Shilingi Trilioni Moja Bilioni Mia Moja Ishirini na Tatu Milioni Mia Mbili Tisini na Tisa na Mia Moja Hamsini na Nne Elfu (Shilingi 1,123,299,154,000) ni fedha za nje” Alisema Waziri Kairuki.