BIL.16 KUNUNUA MAGARI 81, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA, WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUNUFAIKA

“TAMISEMI imetengewa Tsh. Bilioni 16.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa “Kati ya magari hayo, magari 5 ni ya Wakuu wa Mikoa, magari 2 ni ya Makatibu Tawala wa Mikoa na magari 74 ni ya Wakuu wa Wilaya” Mhe. Angela Kairuki.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Angela Kairuki amesema hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha wa 2023/2024 leo April 14, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.


Waziri Kairuki pia amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetengewa Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa boti 4 katika Halmashauri za Wilaya za Ludewa, Buchosa, Nyasa na Sumbawanga ili kuimarisha doria, ulinzi na ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri hizo.


“Hadi Februari, 2023, Tume imepokea Shilingi Bilioni 7.83. Majukumu yaliyotekelezwa ni pamoja na kusajili walimu 9,800, kupandishwa vyeo walimu 1,003, Walimu 3,347 wamethibitishwa kazini na Walimu 3,388 wamebadilishiwa vyeo” Alisema Waziri Kairuki.


“Kuhuisha TANGE za walimu kwenye Wilaya zote 139, vikao 300 vya mashauri ya nidhamu kwa walimu vya kisheria vimefanyika, Mashauri 273 ya nidhamu ya walimu yamefanyiwa uchunguzi na kuwasilishwa kwenye Kamati za Wilaya kwa ajili ya kutolewa uamuzi”Alisema Mhe. Kairuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *