UKOSEFU WA UMEME KUFIKIA UKOMO JIMBO LA HAI

Serikali Kupitia wizara ya ya Nishati imejidhatiti kukamilisha zoezi la kuwasambazia wananchi umeme katika Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro ndani ya kipindi cha cha miezi miwili.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato Leo April, 13, 2023 Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Mafuwe alilouliza kuwa “Serikali ilituahidi kutuletea Mkandarasi kwaajili ya kukamilisha Vitongoji 47 vilivyoko ndani ya Jimbo la Hai, Ni lini Mkandarasi huyo ataanza kazi kwenye vitongoji hivi?” Alisema Mhe. Mafuwe

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Wizara hiyo amekiri kuwepo kwa utaratibu wa kumpata Mkandarasi wa Kwenda kukamilisha Umeme katika maeneo ya Hai na maeneo mengine ya Kilimanjaro.

“Ni kweli taratibu za kumpata Mkandarasi wa kwenda kukamilisha umeme katika maeneo ya Hai na maeneo mengine ya Kilimanjaro ambayo yalikuwa yameshamaliza hatua ya Vijiji, yanaendelea na katika miezi miwili ijayo Mkandarasi atakuwa amepatikana na ataenda kuingia saiti kwaajiji kuweza kupeleka umeme katika maeneo hayo ambayo yalikuwa hayajafikiwa na umeme. Alisema Mhe. Byabato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *