RAIS SAMIA ATOA AJIRA 21,200 ZA ELIMU NA AFYA

OR- TAMISEMI

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za Ualimu na Afya. Idadi ya Watumishi watakaoajiriwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi na Sekondari. Aidha idadi ya watumishi watakaoajiriwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauro, Vituo vya Afya na Zahanati”.

Angellah Kairuki
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI
12.04.2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *